Hosea 2:18-23


18 aKatika siku ile nitafanya Agano kwa ajili yao
na wanyama wa kondeni, na ndege wa angani,
na viumbe vile vitambaavyo ardhini.
Upinde, upanga na vita,
nitaondolea mbali katika nchi,
ili kwamba wote waweze kukaa salama.

19 bNitakuposa uwe wangu milele;
nitakuposa kwa uadilifu na haki,
kwa upendo na huruma.

20 cNitakuposa kwa uaminifu,
nawe utamkubali Bwana.


21 d“Katika siku ile nitajibu,”
asema Bwana,
“nitajibu kwa anga,
nazo anga zitajibu kwa nchi;

22 enayo nchi itajibu kwa nafaka,
divai mpya na mafuta,
navyo vitajibu kwa Yezreeli.

23 fNitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe;
nami nitaonyesha pendo langu kwake
yule ambaye nilimwita, ‘Si mpenzi wangu.
Kiebrania ni Lo-Ruhama.

Nitawaambia wale walioitwa, ‘Sio watu wangu,’
Kiebrania ni Lo-Ami.

‘Ninyi ni watu wangu’;
nao watasema, ‘Wewe ndiwe Mungu wangu.’ ”
Copyright information for SwhKC